
Harry Kane ameambiwa akatae kusaini mkataba mpya Tottenham, huku Bayern Munich wakimsarandia mshambuliaji huyo wa England mwenye miaka 29.
Crystal Palace itapeleka ofa ya £20m kwa ajili ya kiungo wa Chelsea na England Conor Gallagher, 22, mwezi Januari January, baada ya kufanya vyema Selhurst Park msimu uliopita alipokuwa anacheza kwa mkopo.

Familia ya Glazer imeweka bei ya £3.75bn kwa timu yao ya Manchester United, na hilo linaweza kuwavutia wanunuzi toka Dubai.

Mlinzi wa Arsenal na timu ya taifa ya Ureno chini ya miaka 21 Nuno Tavares, 22, alisema alitaka iweke kioengele cha kununuliwa kwenye mkataba wake wa mkopo Marseille.
Arsenal haikukaribia kumsajili kiungo wa Leicester mbelgiji mwenye miaka 25 Youri Tielemans licha ya kuhusishaa na uhamisho huo wa £25m.

Bayern Munich inamtaka kinda wa miaka 18 wa Barcelona na Hispania Gavi, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao.
Leeds itajaribu tena kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven na Uholanzi Cody Gakpo, 23 mwezi Januari, baada ya kushimdwa kumsajili dirisha la sasa la kiangazi.

Juventus inatarajiwa itapeleka ofa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Brazil Roberto Firmino, 30, mwezi Januari.
Galatasaray inataka kumsajili mlinzi wa Uturuki Caglar Soyuncu, 26, kabla ya kifungwa kwa dirisha lao la usajili wiki ijayo baada ya kuwekwa nje ya kikosi cha Leicester kikichocheza na Brighton Jumapili.

Chelsea bado haijampata mkurugenzi wa michezo huku mlinzi wa zamani wa Barcelona Maxwell na mwingine wa Liverpool Michael Edwards wakiwa kwenye orodha ya wanaowania nafasi hiyo.

Lucas Moura yuko tayari kumalizia mkataba wake na kuondoka Tottenham kama mchezaji huru mwaka 2024 baada ya ofa zilizokuja siku ya mwisho wa usajili kutoka Newcastle na Aston Villa kwa ajili ya winga huyo mbrazil mwenye miaka 30 kukataliwa.
Chelsea iko kwenye nafasi nzuri ya kunsajili winga kinda wa Urusi Arsen Zakharyan,19 kutoka Dinamo Moscow, anayewaniwa pia na Barcelona na Real Madrid.