Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Dorothy Gwajima atembelea soko Kuu la Majengo Jijini Dodoma tarehe 28 Septemba, 2022 ambako amekutana na baadhi ya wafanyabiashara kwa lengo la kukusanya maoni ya namna ya kutatua tatizo la watoto wanaoomba mitaani na kwenye mikusanyiko mbalimbali.