Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amkabidhi Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe Tuzo ya mshindi wa Kwanza ya Ubunifu wa programu ya kuwasaidia Vijana katika sekta ya kilimo. Wizara ya Kilimo imeshinda tuzo hiyo iliyotolewa na Baraza la Taifa la Uwekezaji katika Kongamano la 6, lililofanyika tarehe 19 Septemba, 2022 Jijini, Dodoma.