ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, February 7, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI NMB MARATHON OKTOBA MOSI

I am Krantz by I am Krantz
Sep 22, 2022
in HABARI
0
WAZIRI MKUU MAJALIWA  MGENI RASMI NMB MARATHON OKTOBA MOSI
0
SHARES
85
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

Waziri Dkt. Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Waziri Dkt. Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Jan 25, 2023

🔴 #LIVE : NMB AWARDS SHOWCASE – NOV 23, 2022

Nov 23, 2022

NMB yapongezwa kusaidia Wakandarasi- Zanzibar

Nov 16, 2022
Load More
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

 

Afisa Mkuu Raslimali watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay akizungumza wakati wa kutambulisha Jezi na Medali zitakzotumika kwenye NMB Marathon, kutoka kushoto ni Nahodha msaidizi wa NMB Joging Club, Stella Moto, Mkuu wa Idara ya Bima, Martine Masawe na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya NMB Marathon Mercy Nyange.

Raslimali watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonnay, Mkuu wa Idara ya  Bima Martine Massawe, Mwenyekiti Kamati ya Maaandalizi ya NMB Marathon, Mercy Nyange (kulia) na  kushoto ni Nahodha msaidizi wa NMB Joging Club Stella  Motto wakionyesha jezi na Medali zitazotumika kwenye mbio za NMB Marathon zitakayofanyika tarehe moja mwezi wa kumi katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam.


LICHA ya washiriki zaidi ya 3,000 kujisajili kushiriki Mbio za Hisani za NMB Marathon 2022, Benki ya NMB imeeleza sababu za kusogezwa mbele kwa mbio hizo, huku ikitambulisha medali na jezi zitakazovaliwa, pamoja na kumthibitisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa Mgeni Rasmi.

LICHA ya washiriki zaidi ya 3,000 kujisajili kushiriki Mbio za Hisani za NMB Marathon 2022, Benki ya NMB imeeleza sababu za kusogezwa mbele kwa mbio hizo, huku ikitambulisha medali na jezi zitakazovaliwa, pamoja na kumthibitisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa Mgeni Rasmi.NMB Marathon zitafanyika Oktoba Mosi badala ya Septemba 24 kama ilivyokuwa imepangwa awali, zikianzia na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders Cub, Kinondoni jijini Dar es Salaam, lengo likiwa kukusanya Sh. Milioni 600 za kusaidia matibabu ya kinamama wenye Fistula kwenye Hospitali ya CCBRT.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa fulana na medali hizo, Afisa Mkuu wa Rasirimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay, alisema hadi jana asubuhi zaidi ya washiriki 3000 wamejisajili na kuwa vifaa ‘kits’ vilivyoandaliwa kwa wakimbiaji hao ni vya ubora wa kimataifa.

Alibainisha kuwa, katika kujiweka sawa kwa mbio hizo, NMB ilifanya bonanza la NMB na Wabunge wiki jana, ambalo wamelitumia kama maandalizi, ushawishi na mialiko kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili waweze kuwa sehemu ya washiriki wa mbio hizo.

“Tunaamini wabunge hao ni miongoni mwa watakaonufaika na uamuzi huu wa kusogeza mbele, ambao umetokana na maombi ya wengi miongoni mwa Watanzania, kututaka tusogeze ili waweze kushirikiana nasi katika tukio hili, linaloenda kurejesha tabasamu kwa kinamama wenye Fistula.

“Kwa hiyo usajili unaendelea Mbezi Beach, Juliana Pub iliyopo Mtana Bar pale Kanisa la St. Peters, Mlimani City na kwenye tovuti ya marathon.nmbbank.co.tz. Watanzania wazidi kujisajili na waliofanya hivyo tayari, wafike kuanzia kesho (leo) Mlimani City kuchukua ‘kits’ zao,” alifafanua Akonaay.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya NMB Marathon, Mercy Nyange, alibainisha kwamba benki yake inashukuru kupata wadhamini wengi waliojitokeza kudhamini mbio hizo ili kuunga mkono jitihada za kulikomboa kundi la kinamama, wanaokabiliwa na changamoto hiyo.

Mercy aliwaomba Watanzania walioomba kuongezwa kwa muda wa usajili kujitokeza na kwamba udhamini mnono kutoka Sanlam, UAP, Toyota na kampuni nyinginezo, unawahakikishia zawadi nzuri kwa washindi wa kwanza hadi wa 10 kategori zote za kilomita 5, 10 na 21, pamoja na mbio za watoto.

“Niweke msisitizo tu, kama ilivyosemwa washiriki zaidi ya 3,000 wamejisajili hadi sasa, kwahiyo fursa hii iliyoombwa itumiwe vizuri na watu wajitokeze kujisajili katika maeneo yaliyotajwa hapo juu,” alisisitiza Mercy.

 

Related

Tags: NMB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumanne Februari 7,2023

by ALFRED MTEWELE
Feb 7, 2023
CONTE AMPIGIA SIMU KANE BAADA YA KUIFUNGA CITY
HABARI

CONTE AMPIGIA SIMU KANE BAADA YA KUIFUNGA CITY

by Shabani Rapwi
Feb 6, 2023
MAN CITY YASHTAKIWA, KUPUNGUZWA POINTI AU KUSHUSHWA DARAJA
HABARI

MAN CITY YASHTAKIWA, KUPUNGUZWA POINTI AU KUSHUSHWA DARAJA

by Shabani Rapwi
Feb 6, 2023
TIGO KWENDA KUMKABIDHI  GARI MSHINDI WA NDINGA LA KISHUA
HABARI

TIGO KWENDA KUMKABIDHI GARI MSHINDI WA NDINGA LA KISHUA

by ALFRED MTEWELE
Feb 6, 2023
SHOTI YA UMEME YAUA MAMA AKIMUOKOA MTOTO WAKE
HABARI

SHOTI YA UMEME YAUA MAMA AKIMUOKOA MTOTO WAKE

by Shabani Rapwi
Feb 6, 2023
AFARIKI KWA KULA CHAKULA CHENYE SUMU
HABARI

AFARIKI KWA KULA CHAKULA CHENYE SUMU

by Shabani Rapwi
Feb 6, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
September 2022
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930  
« Aug   Oct »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In