ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, February 7, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

WAZIRI MKUU MAJALIWA “VIASHIRIA VYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI VIDHIBITIWE”

Kilimanjaro, Tanzania

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Sep 22, 2022
in HABARI
0
WAZIRI MKUU MAJALIWA “VIASHIRIA VYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI VIDHIBITIWE”
0
SHARES
54
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

Waziri Mkuu: Msirekodi matukio na Kuweka Mitandaoni, Pelekeni Mamlaka Husika

Waziri Mkuu: Msirekodi matukio na Kuweka Mitandaoni, Pelekeni Mamlaka Husika

Feb 2, 2023

MAJALIWA- MIRADI 630 YA UWEKEZAJI INAYOGHARIMU SH. BIL. 3.68 YASAJILIWA NA TIC

Jan 20, 2023

WAZIRI MKUU AFANYA UKAGUZI HIFADHI YA USANGU

Jan 17, 2023
Load More
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji wote Serikalini kuweka mkakati wa kudhibiti viashiria vyote vya uvunjifu wa amani katika maeneo yao.
Mheshimiwa Majaliwa amesema lengo la agizo ni kusisitiza utekelezwaji wa maono na dhamira ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa katika hali ya utulivu ili kuendelea kufikisha maendeleo katika kila eneo.
Amesema hayo jana (Jumatano, Septemba 21, 2022) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani yayofanyika katika ukumbi ya Kuringe, Moshi Kilimanjaro.
“Hatuna budi kuitunza amani yetu kulingana na umuhimu wake kwani amani ni tunda la upendo, utulivu, mshikamano na maridhiano.”
Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za kikanda na kimataifa katika kutafuta na kudumisha amani na usalama.
“Jukumu la kudumisha amani na kuilinda amani ni ajenda ya kidunia inayomgusa kila mmoja, ili kulinda ustawi wa vizazi vya leo na kesho.”
Pia, amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendelea kuchukua hatua na tahadhari zote zinazohitajika ili kuendelea kudumisha amani nchini.
“Serikali ya Awamu ya Sita, inafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha amani na usalama vinadumishwa kwa kuweka mikakati mbalimbali ya maendeleo inayolenga kutokomeza umaskini. Umaskini ni chanzo kikubwa cha migogoro sehemu nyingi duniani kwa sababu watu wanagombania kufaidika na rasilimali chache zilizopo.”
Ameongeza kuwa kila palipo na amani, shughuli za kiuchumi na kijamii hufanyika kwa ufanisi mkubwa na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi na ustawi wa wananchi kwa ujumla. “Niwasihi wananchi kuendelea kutunza na kuilinda tunu ya amani tuliyojaliwa hapa nchini”
“Ni lazima tuendelee kuilinda amani nchini kwetu, Watanzania tuendelee kudhibiti yeyote mwenye nia ya kuiharibu amani yetu. Jukumu la kuilinda amani hii ni agenda yetu sote, tuitekeleze.”
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: OFISI YA WAZIRI MKUU
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

HIZI HAPA JEZI MPYA ZA SIMBA ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
HABARI

HIZI HAPA JEZI MPYA ZA SIMBA ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023
TANZANIA, UAE ZASAINI KUHIFADHI MAZINGIRA
HABARI

TANZANIA, UAE ZASAINI KUHIFADHI MAZINGIRA

by ALFRED MTEWELE
Feb 7, 2023
YANGA KWENDA TUNISIA LEO NA WACHEZAJI 25
HABARI

HAMTAMUONA KOCHA NABI AIRPORT – ALLY KAMWE

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023
YANGA KWENDA TUNISIA LEO NA WACHEZAJI 25
HABARI

YANGA KWENDA TUNISIA LEO NA WACHEZAJI 25

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023
QUEIROZ KOCHA MPYA QATAR
HABARI

QUEIROZ KOCHA MPYA QATAR

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023
ATSU APATIKANA AKIWA HAI KUTOKA KWENYE VIFUSI
HABARI

ATSU APATIKANA AKIWA HAI KUTOKA KWENYE VIFUSI

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
September 2022
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930  
« Aug   Oct »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In