Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa Ripoti ya Tume ya Lancet Oncology Kuhusu Udhibiti wa Saratani kwa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara Barani Afrika. Uzinduzi huo umefanyika eneo la Hyatt Regency leo Septemba 26, 2022 ambapo wadau mbalimbali wa afya wamejumuika na Wageni waliowasili kutika Nchi za nje kushiriki tukio hilo. Waziri Ummy pamoja ya kwamba alikuwa Nchini MAREKANI akiendeleza jitihata za kuja na mbimu mbadara za kuboresha utoaji bora wa huduma za Afya, amesema bado imembidi kurejea kwa uharaka zaidi maana limekuwa ni jambo la msingi kutokana na kuonekana kuwa bila ya kutolewa kwa chanjo au suluhu ya mapema kutakuwa na shambulio kubwa la Saratani kwa binadamu ifikapo mwaka 2030. Hivyo serikali kupitia wizara ya Afya itaanzisha Kampeni ya Udhibiti wa Magonjwa ya Ukimwi, yasiyoambukizwa na Ini ili kuweza kuokoa maisha ya wengi.