Kampuni ya Adidas imetangaza kuvunja mkataba wa ushirikiano wake na Rapper Ye (Kanye West) leo October 25 na kusema Kampuni hiyo haiwezi kuvumilia chuki au aina yoyote ya matamshi ya chuki na kusisitiza kuwa haikubaliani na kauli za Kanye West za hivi karibuni akihojiwa kwenye podcast ya “Drink Champs” na kusema “naweza kusema kauli yeyote dhidi ya Wayahudi na Adidas haiwezi kuniacha”.
–
Sasa ni ramsi kwamba kuanzia sasa uuzaji na uzalishaji wa bidhaa zenye chapa ya ‘Yeezy’ umesimamishwa pamoja na malipo yeyote kwa Ye na kampuni zake pia umesimamishwa ambapo Adidas imesema itapata hasara ya $246 milioni kwa uamuzi huo.
–
Kampuni ya Adidas imefanya kazi na Kanye West kuanzia mwaka 2013 lakini Adidas iliweka ushirikiano huo chini ya ukaguzi mapema mwezi huu baada ya Ye kuonekana hadharani akiwa amevaa T-shirt iliyoandikwa “White Lives Matter” ambapo ukiachia Adidas, Kampuni nyingine zilizovunja uhusiano wake na Rapper Kanye ni pamoja na Balenciaga pamoja na jarida maarufu la mitindo Vogue.