Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 33 kunusurika kutokana na ajali iliyohusisha magari matatu ikiwemo gari dogo, Mitsubishi lenye namba za usajili T846 CWN, lori na basi kampuni ya BM COACH yenye namba ya usajili T 959 DDE kugongana katika eneo la Makunganya barabara kuu ya Morogoro – Dodoma.
–
Kwa mujibu wa kaimu mkaguzi wa jeshi la zimamoto na uokoaji, Ahmed Lemba amesema ajali hiyo imetokea majira ya mchana na kusababisha kifo cha dereva wa gari dogo Alphonce aliyekuwa akitokea Morogoro kwenda Dodoma ambaye alibanwa na magari mawili na kusababisha kifo hicho.
–
Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori kusimamisha lori lake katikati ya barabara na kusita kuendelea mara baada ya kutaka kuyapita magari mengine na kusabisha gari dogo la MISTUBISHI kubanwa na basi la kampuni ya BM.