Afisa habari wa klabu ya Yanga SC ametolea ufafanuzi taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kufukuzwa kwa kocha wao Nasreddine Nabi kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
–
Ali Kamwe amesema mwamba taarifa zinazosambaa ni mawazo na mitazamo ya wachambuzi wa soka hapa nchini na siyo msimamo wala mawazo ya uongozi wa klabu hiyo na hivyo basi wao wanamtambua Nabi kama kocha wao na hawana mpango wa kumfukuza kocha huyo.
ADVERTISEMENT