Meneja wa Benki ya Biashara ya Akiba Tawi la Mbagala, Erick Kuyeko akifanya usafi pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Kibonde Maji katika kuadhimisha siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Kibonde Maji jijini Dar es Salaam leo. ACB imeshiriki kampeni hiyo ikiwa ni mwendelezo wa kurudisha fadhila kwa kusaidia jamii kufanya usafi pamoja na wakazi wa eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akizungumza na wakazi wa Mbagala Kibonde Maji baada ya kumaliza kufanya usafi katika kuadhimisha siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata hiyo jijini Dar es Salaam leo. Benki ya Biashara ya Akiba imeshiriki kampeni hiyo ikiwa ni mwendelezo wa kurudisha fadhila kwa kusaidia jamii kufanya usafi pamoja na wakazi wa eneo hilo.
Ofisa Masoko wa Benki ya Biashara ya Akiba, Anthony Kunambi ( kushoto) na Meneja wa Tawi la Mbagala, Erick Kuyeko wakiongozana na wanafunzi wa shule ya msingi Kibonde Maji katika kuadhimisha siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Kibonde Maji jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Masoko wa Benki ya Biashara ya Akiba, Anthony Kunambi akifanya usafi pamoja na wakazi na wafanyabiashara wa Kibonde Maji katika kuadhimisha siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Kibonde Maji jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya Akiba wakishiriki kufanya usafi katika stendi mpya ya mwendo kasi ya Mbagala Kibonde Maji wakati wa kuadhimisha siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Kibonde Maji jijini Dar es Salaam leo. ACB imeshiriki kampeni hiyo ikiwa ni mwendelezo wa kurudisha fadhila kwa kusaidia jamii kufanya usafi pamoja na wakazi wa eneo hilo.