
Benki ya CRDB imeendesha semina maalum kwa wateja wake wakubwa juu ya mfumo wa huduma ya benki kupitia mtandao ‘Internet Banking’ iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Meneja Mwandamizi wa Njia Mbadala za Ufikishaji Huduma kwa Wateja, Mangire Kibanda amesema Benki hiyo imefanya maboresho makubwa katika huduma ya ‘Internet Banking’ yanayowawezesha wateja kufanya miamala ya kifedha popote pale walipo.


ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT