Timu ya Biashara kutoka Benki ya CRDB kanda ya Kaskazini imeenea mtaani ili kusogeza huduma mbalimbali stahiki za kibenki,ikiwemo kukufungulia akaunti maalum ya kwa ajili ya matumizi binafsi, pamoja na kumfahamisha kuhusu huduma mbalimbali na bidhaa bunifu zinazopatikana kupitia benki hio.
Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Bi. Chiku Issa amesema kwamba wamejipanga kuhakikisha wananchi wote wanajumuishwa kwenye mfumo rasmi wa sekta ya fedha. “Kama benki ya Kizalendo tunao wajibu wa kuhakikisha wananchi na wateja wetu wanapata fursa ya kuelewa huduma zetu kwa ufasaha kabisa na hivyo kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla” alisisitiza Meneja wa kanda huyo.