Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wameungana kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya hio, Abdulmajid Nsekela kwa kutunikiwa tuzo ya Mwanachama wa Heshima wa Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB) kutokana na mchango wake katika Sekta ya Benki na Fedha nchini kupitia hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Sekta ya Benki na Fedha .
Aidha, wametoa pongezi pia kwa Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa Benki, Dkt. Charles Kimei kwa kutunikiwa tuzo hiyo ya Mwananchama wa Heshima na TIOB kutokana na mchango wake katika sekta ya Benki na Fedha.
Hii ni ishara ya kuonyesha jinsi gani Benki ya CRDB imekua na uongozi mahiri miaka hadi miaka.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT