ADVERTISEMENT

Benki ya CRDB hii leo imeshiriki katika Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Afya ya Akili lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam ambalo lilifunguliwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Akizungumza katika Kongamano hilo Mkuu wa Kitengo cha Masoko Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda amesema benki inajivunia kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jitihada za Serikali za kuboresha sekta ya afya nchini.
Kamuhanda amesema Benki imekuwa ikifanya ufadhili wa miradi ya afya inayotekelezwa na Serikali pamoja na sekta binafsi, ambapo hadi sasa zaidi ya shilingi bilioni 100 zimetolewa.
Aliongezea kuwa Benki hio pia imekuwa ikifanya uwekezaji kupitia sera ya uwekezaji kwa jamii ambapo kipaumbele kikubwa kinatolewa katika sekta ya afya.
ADVERTISEMENT