Benki Exim Tanzania yatoa madawati 100 katika mkoa wa Tanga, Madawati hayo yalikabidhiwa na Mtendaji Mkuu wa Benki hio Bw. Jaffari Matundu na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba. Hafla hii pia ilihudhuriwa na viongozi wengine waandamizi wa mkoa wa Tanga akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Pili Mnyema na Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi Newaho Mkisi pamoja baadhi ya wafanyakazi wa benki hio. Hii ni kufanya muendelezo wa kampeni yake ya ugawaji wa madawati 1000 kwa shule za Msingi Tanzania iliyozinduliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi 10 mwaka jana.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT