ADVERTISEMENT
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) tawi la Mwanza imetoa msaada wa mifuko ya saruji 200 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Samia iliyoko wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza sambamba na msaada wa madawati 50 kwa ajili ya shule za Msingi zilizopo wilayani Ilemela mkoani humo ikiwa ni hatua ya Benki ya NBC katika kuunga mkono juhudi za Serikali pamoja na wananchi katika kuboresha elimu wilayani humo.
Akizungumza kwenye hafla za kukabidhi misaada hiyo, Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mwanza Bw. Thomas Lijaj alisema misaada hiyo inalenga kuunga mkono jitihada ambazo tayari zinaendelea kuonyeshwa na Serikali pamoja na wananchi katika maeneo husika kwa kuboresha miundombinu ya elimu.
“Tunaamini kwamba mifuko ya saruji pamoja na madawati tuliyoikabidhi katika halmashauri hizi mbili zitasaidia kuunga mkono jitihada ambazo tayari zipo katika kutatua changamoto zilizopo za uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule husika. Lengo ni kuwasaidia wanafunzi wapate mazingira bora zaidi ya kujifunzia,’’ alisema Bw Lijaj.


ADVERTISEMENT