ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

BENKI YA NMB KINARA WA USAWA WA KIJINSIA AFRIKA

I am Krantz by I am Krantz
Oct 27, 2022
in HABARI
0
BENKI YA NMB KINARA WA USAWA WA KIJINSIA AFRIKA
0
SHARES
34
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

–

Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la IFC, Frank Ajilore (watatu kulia) wakionyesha hati ya kutambulika ya Uimara wa Kiuchumi na Usawa wa Kijinsia iliyotolewa kwa benki ya NMB na taasisi ya The EDGE (Economic Dividends for Gender Equality) Certified Foundation. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa masuala Jinsia wa IFC Afrika, Anne Kabugi, kushoto ni Afisa Mkuu Huduma Shirikishi wa NMB, Nenyuata Menjooli na wapili kushoto ni Afisa Mkuu wa Udhibiti NMB, Doreen Joseph.

Ubaguzi wa kijinsia ni mwiko kwa Benki ya NMB na juhudi zake za kutokomeza kabisa unyanyapaaji huo nchini zimeiheshimisha duniani na kupelekea harakati zake za kupambania usawa wa kijinsia kazini kuthibitishwa rasmi kimataifa.

Benki hiyo imetunukiwa na taasisi ya The Edge Certified Foundation hati maalumu ya kutambulika rasmi duniani kama kinara katika mgawanyo wa kiuchumi kwenye suala la kijinsia (EDGE Certification) miongoni mwa taasisi za kifedha barani Afrika.

ADVERTISEMENT



NMB ni ya kwanza kupata mafanikio hayo kitaasisi kwenye nchi zote zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara. Bw Akonaay alisema zipo taasisi nyingine mbili ambazo si za kifedha zenye hati hiyo za Kaskazini mwa Afrika (Moroco na Misri).

Aidha, tafiti zimedhibitisha kuwa uwiano wa kijinsia ni kichocheo kizuri cha ubunifu na ukuaji wa kiuchumi, kuimarika kwa shughuli za uzalishaji mali na kuwepo utulivu wa kifedha na uwiano wa kipato.

RelatedPosts

MORGAN HERITAGE KUACHIA ALBUM YAO APRILI 21

MORGAN HERITAGE KUACHIA ALBUM YAO APRILI 21

Mar 24, 2023

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Ijumaa Machi 24,2023

Mar 24, 2023

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

Mar 23, 2023
Load More



Pia NMB inatambua kuwa swala hili ni miongoni ya vipaumbele vya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa. Bw Akonaay alisema umuhimu wake kimaendeleo ni pamoja na kuzingatia ukuaji wa biashara za kibenki.

Alibainisha faida nyingine za cheti cha EDGE Access ambayo ni hatua ya kwanza ya taasisi kuelekea kufanikiwa kuutokomeza kabisa ubaguzi wa kijinsia ni pamoja na NMB kutambulika kama muajiri anayezingatia masuala ya usawa wa kijinsia kazini.

Naye, Mwakilishi wake mkazi, Bw Frank Ajilore, alisema usawa wa kijinsia kazini kuna faida nyingi kibiashara na kiuchumi kwani akina mama wakiwezeshwa wanachangia vizuri kasi ya maendeleo.

Benki ya NMB yenye wafanyakazi zaidi ya 3,500 imepiga hatua kubwa kwenye eneo hili na uwiano wake wa kijinsia umepanda kutoka asilimia 45 wanawake na asilimia 55 wanaume mwaka 2015 hadi asilimia 48 kwa 52 mwaka huu.

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Ijumaa Machi 24,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
October 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Sep   Nov »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In