Benki ya NMB ikiwa mstari wa mbele kwa ubunifu katika sekta ya TEHAMA kwa kutoa masuluhisho mbalimbali kwa wateja wake wa nyanja zote. Jana imemeshiriki katika Kongamano la sita la TEHAMA (Tanzania Annual ICT Conference) linalofanyika kwa mara ya kwanza Visiwani Zanzibar na kuzinduliwa na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Kauli mbiu ya kongamano hilo ni Mabadiliko ya Kidijitali kwenye Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi.
Benki hio ikiwakilishwa na Mkaguzi Mkuu wake wa Ndani – Benedicto Baragomwa, imetumia fursa ya kongamano hilo kufanya wasilisho kwa washiriki zaidi ya 500 wakiwemo viongozi wa serikali, watalaam wa TEHAMA, wadau wa maendeleo pamoja na wawekezaji katika seka ya TEHAMA kutoka ndani na nje ya nchi kuonyesha uwezo, utayari na ushiriki wetu katika kuwawezesha wananchi kutumia fursa zinazotokana na uchumi wa buluu.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT