
Benki ya NMB imezindua rasmi kampeni yake ya Teleza Kidijitali itakayokuwezesha kufanya miamala au kupata mkopo kiurahisi ukiwa na simu yako ya mkononi tu. Uzinduzi huo ulihuzuriwa na Afisa Mtendaji mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa Mgeni rasmi, na wadau wengineo wengi waliopata nafasi ya kufika hapo.
Benki hio imetambulisha rasmi huduma zifuatazo:
Mshiko Fasta – Huduma hii inamuwezesha mteja wetu kujipatia mkopo wa hadi shilingi laki tano kwa uharaka na urahisi kupitia simu yake ya mkononi bila kufika tawini na bila kuweka dhamana yoyote. Huduma hii inapatikana kupitia NMB Mkononi APP au USSD (*150*66). Mkopo huu unaweza kurejeshwa ndani ya siku 1, 7, 14, 21 au 28 na riba yake itategemea kiwango kilichokopwa.
NMB Pesa Wakala – Huduma ya wakala atakayetumia simu yake ya mkononi kuwa wakala wa Benki ya NMB na kuwawezesha wateja wetu kuweka na kutoa pesa kupitia simu zao kama walivyo mawakala wa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu. Ni rahisi kuwa wakala, unachohitaji ni; simu (janja au kitochi), leseni ya biashara na kitambulisho cha taifa.
NMB Lipa Mkononi – Huduma ya malipo kwa njia ya QR code au Lipa namba inayomuwezesha mfanyabiashara kupokea malipo kwa njia za kidijitali. Suluhisho hili linaruhusu kupokea malipo kutoka makampuni yote ya simu na benki ambazo zimeunganishwa na mtandao wa Mastercard au VISA.
Piga *150*66# au pakua app ya NMB Mkononi uweze kuteleza na huduma hizi. Safari hii ushindwe wewe tu.
Afisa mtendaji wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akiongea katika Hafla ya Uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Teleza Kidigitali.
Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya TELEZA KIDIGITALI Iliyoanzishwa na Benki ya NMB.
Related