Vifo vya watoto 99 nchini Indonesia vimeilazimu nchi hiyo kusimamisha mauzo ya dawa zote zilizo kwenye umbo la vimiminika.
–
Uamuzi huu umekuja wiki chache baada ya dawa za Kikohozi na Mafua kuhusishwa na vifo vya watoto 66 nchini Gambia.
–
Serikali ya Indonesia imesema kuwa dawa hizo zimekutwa na kemikali zinazohusishwa na majeraha ya papo hapo ya figo, tatizo ambazo limesababisha vifo vya watoto 99 tangu kuanza kwa mwaka huu.
–
Hadi sasa kumekuwa na kesi takribani 200 za tatizo hilo kwa watoto, wengi wao wakiwa chini ya miaka mitano.
–
Mapema mwezi huu, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa tahadhari ya Kimataifa kuhusiana na dawa nne za kikohozi na mafua. Shirika hili lilikuta dawa hizo zikiwa na kiasi “kisichokubalika” cha kemikali mbili.
–
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Indonesia, kemikali hizohizo sasa zimekutwa kwenye baadhi ya dawa nchini humo, hata hivyo hakutaja majina ya dawa husika.