Msemaji wa Simba, Ahmed Ally amesema kikosi cha Primeiro de Agosto ya Angola 🇦🇴 kitatua Tanzania 🇹🇿 Oktoba 14 kuikabili Simba Jumapili katika uwanja wa Mkapa mechi ya marudiano baada ya kufungwa mabao 3-1 nyumbani. Ally amewataka mashabiki wa timu hiyo kukata tiketi mapema ili kuwahi na kuujaza uwanja wa Mkapa.
ADVERTISEMENT
“Wageni wetu Primeiro de Agosto watawasili nchini Oktoba 14 majira ya mchana, kwa wale ambao wangependa kwenda kuwapokea wanakaribishwa uwanja wa ndege. Waamuzi wanatokea Afrika Kusini na watawasili nchini siku hiyo hiyo ya Oktoba 14.” Alisema Ahmed Ally.
ADVERTISEMENT