Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz amesema hawezi kumuoa Zuchu maana ni Msanii wake.
–
Kauli ya Diamond inakuja baada ya Babu Tale kumwambia aoe kufuatia kuposti video akibusiana na Zuchu.
–
“Sasa nitamuoaje wakati ni Msanii wangu Bosi, hilo busu hapo lisiwatishe viongozi, ni salamu tu za Kijerumani” amesema Diamond.
–
Utakumbuka wawili hao ambao wametoa pamoja ngoma tatu, Litawachoma, Cheche na Mtasubiri, wamekuwa wakidaiwa kuwa na mahusiano.