Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kipanga, amesema kuwa katika sera mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadaye, elimu ya msingi itakomea darasa la 6 na hakutakuwa na mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi na kwamba mtihani utakuwa ni kidato cha nne tu.
–
“Katika sheria na sera hii ijayo, elimu ya msingi itaishia darasa la 6 na hakutakuwa na mtihani wa Taifa bali tutakuwa na course assessment, baada ya kufaulu mwanafunzi atajiunga na kidato cha kwanza hadi cha nne ambapo atakuwa tayari na mchepuo rasmi,”- Naibu Waziri Kipanga
–
Aidha Naibu Waziri ameongeza kuwa, “Kama ni kilimo ni kilimo, hakuna kusoma vitu vyote na tutakuwa na michepuo karibu 15 hivi, tunalenga huyu kijana akihitimu kidato cha 4 awe na uwezo wa kuwa na maarifa fulani na ujuzi ili aajirike au aajiriwe kama hatakwenda kidato cha 5”.