Beki wa Real Madrid, Antonio Rudiger amethibitisha kuwa anaendelea vizuri na kuwashukuru wote waliompa pole baada ya kujeruhiwa na kipa wa klabu ya Shakhtar, Anotolii Trubin wakati akifunga bao la kusawazisha.
–
Kupitia ukurasa wake wa mtandaonwa kijamii wa Instagram, Rudiger ameandika “Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvu zaidi 👊🏾 Niko sawa – asante kwa jumbe zenu🙏🏾 #Amini Daima”
ADVERTISEMENT
Rudiger alifunga bao hilo lililoipeleka Madrid hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya katika dakika tano za nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika.
ADVERTISEMENT