Msanii Maarufu na mkurugenzi mkuu wa Label ya Konde Music Worldwide hapa nchini, Harmonize (Rajab Abdul Kahali) kupitia historia yake alipenda pia kucheza mpira wa miguu ingawa kipaji cha muziki kimechukua nafasi zaidi na kuua kabisa ndoto ya yeye kuwa mchezaji mkubwa wa soka kutokea hapa nchi. Msanii huyo ajumuika pamoja na kikosi cha Yanga akiwa amevalia jezi namabari 10 inayotumika zaidi na mchezaji wa klabu hio Aziz Ki katika kufanya mazoezi ya kujianda na mechi zinazofuata, amabapo katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara atakipiga dhidi ya mpinzani wa karibu Simba SC kuleta burudani ifahanikayo kama “Derby ya Kariakoo” maana zikutanapo timu hizo mbili nchi husimama na nyasi huchimbika, mechi ambayo itachezwa siku ya Jumapili Oktoba 23, 2022 na nyingine ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya klabu ya AFRICAIN kutokea nchini Tunisia. Hapa unaweza jionea namna msanii huyu anavyoupenda mchezo huu pia.