ADVERTISEMENT
Ukitaka kufanikiwa iga kwa waliofanikiwa. Mpaka sasa Burna Boy ana album sita, Mixtape mbili, EP mbili na single 39. Kila kimoja hapo kilitolewa chini ya usimamizi mzuri, Promotion ya maana ilifanyika na Kila kimoja kikaleta matokeo makubwa.
–
Harmonize ni miongoni mwa wasanii wakurupukaji kuwahi kutokea Tangu Dunia hii iumbwe, Jamaa ametangaza kwamba hivi karibuni ataachia Album, “High School” imetoka hivi karibuni na haijafanya maajabu yoyote lakini mwezi huu anataka kuachia Album nyingine.
–
Diamond hajakupuka kuachia Album, ameamua kwamba atangulize E.P kisha itumike kama Promo kwa ajili ya Album, hivi ndivyo System ya muziki inavyofanya kazi kitaalamu, E.P sometimes hutumika kama Promo na kuwaweka attention watu kwa ajili ya Album. Pia ukweli ni kwamba E.P ya Diamond imefanya vizuri kuliko album ya Harmonize.
–
Haya yote Harmonize hajui, yeye anajua kuachia ngoma tu, inaonekana hana mshauri kabisa na hata kama anashauriwa basi ni kiburi Mbobevu.
–
Sioni kama ni muda muafaka kwa Harmonize kuachia ngoma. Inabidi atulie kwanza, ameshazoeleka sana maana kila Mara anaachia ngoma, hii Album ikitoka itaishia buza tu. Sometimes Harmonize aonee huruma mfuko wake, Hivi vitu vinatayarishwa kwa pesa ndefu sana, then yeye anakurupuka tu kuachia utazani anashindana na mtu.
–
Ameandika hopetygatz kutia kwenye ukurasa wake wa IG
ADVERTISEMENT