Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameachiliwa huru baada ya muda wake wa kutumikia kifungo jela kumalizika kwa makosa ya kudharau Mahakama, Wizara ya sheria imesema.
–
Zuma alihukumiwa miezi 15 jela mwaka jana baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki kwenye uchunguzi kuhusu ufisadi.
–
Alijasilimisha mwenyewe Julai 7 kuanza kutumikia kifungo chake, hali ambayo ilichochea ghasia ambazo Afrika Kusini haijawahi kushuhudia katika miaka kadhaa, wakati wafuasi wake wenye hasira walipoingia barabarani kuandamana.
–
Zuma aliachiliwa huru mwezi Septemba mwaka wa 2021 kutokana na sababu za kiafya. Lakini mwezi Desemba, Mahakama ilifutilia mbali msamaha huo na kuamua arejee jela.