ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

KAGERA YANYOSHEWA KIDOLE, KASI NDOGO

Kagera, Tanzania

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Oct 27, 2022
in HABARI
0
KAGERA YANYOSHEWA KIDOLE, KASI NDOGO
0
SHARES
37
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

DKT. DUGANGE- BILIONI 69.95 ZIMETENGWA KUNUNUA VIFAA TIBA NCHINI

DKT. DUGANGE- BILIONI 69.95 ZIMETENGWA KUNUNUA VIFAA TIBA NCHINI

Feb 9, 2023

Dkt. Jafo: “Huenda zaidi ya Sh. Trilioni 1 Zikapatikana kwa Mwaka Kutokana na Biashara ya Kaboni”

Feb 3, 2023

Bilioni 213 za Miradi ya DMDP Zaistawisha Temeke

Feb 2, 2023
Load More
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za mitaa (USEMI) ikiongozwa na Mhe. Jaffari A. Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala haijaridhishwa na kasi ya Ujenzi wa Shule mpya maalum ya Sekondari ya Bweni na sayansi ya Wasichana katika Mkoa Kagera kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Oktoba 2022 wakati Kamati hiyo ya USEMI ikipokea na kujadili taarifa kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya 10 za wasichana zinazojengwa katika mikoa 10 ya awali ambapo kila mkoa utajengewa shule moja.
“Leo tumepokea taarifa za ujenzi wa shule mpya katika mikoa 10, Wapo waliofikia asilimia 80 lakini Kamati imesikitishwa sana na Mkoa Kagera, ujenzi unaenda taratibu mno na bado wapo chini ya asilimia ambayo tuliitarajia” amesema Chaurembo
Kamati ya USEMI imeuagiza Uongozi wa Mkoa Kagera kuhakikisha wanasimamia mradi wa Ujenzi wa shule hiyo uende kwa kasi inayotakiwa ili ifikapo tarehe 31 Disemba 2022 ujenzi uwe umekamilika kwa ajili ya kupokea wanafunzi Mwezi Januari 2023.
Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya USEMI, Mhe. Jaffari A. Chaurembo amepongeza hatua za ujenzi zilizofikiwa katika mikoa 9 na ameutaka Mkoa Kagera ndani ya siku mbili kuwasilisha mpango kazi kwa kamati wa namna watakavyoweza kukamilisha Ujenzi Shule hiyo kwa Wakati.
Kwa Upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Angellah Kairuki amesema Serikali ilitoa Bilioni 3 kwa kila mkoa katika Mikoa 10 na ikaagiza kufikia tarehe 31 Disemba 2022 Ujenzi wa madarasa na miundombinu yote iwe imekamilika kwa viwango kulingana na miongozo iliyowekwa.
Waziri Kairuki amesema Wizara itahakikisha inaweka kambi katika Mkoa wa Kagera na Mwanza na mikoa mingine ambayo ipo nyuma katika utekelezaji wa Miradi hiyo na akaitaka Mikoa yote ihakikishe inajiwekea mpango kazi ya kukamilisha Ujenzi wa Shule hizo wakati taratibu za usajili zinaendelea.
Vile vile, ametoa wito kwa Mikoa mingine kuanza maandalizi ya Ujenzi wa Shule Mpya za wasichana zitakazojengwa kwa mikoa yote nchini kwa awamu ili kuondokana migongano kama ulivyotokea katika Mkoa wa Tanga na kusababisha fedha hizo kuhamishiwa mkoa wa Njombe.
Ujenzi wa Shule maalum Mpya wa Sekondari za wasichana kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Sita unatekelezwa katika mikoa 10 ya awali ambayo ni Dar es Salaam, Lindi, Ruvuma, Kagera, Songwe, Singida, Pwani, Mwanza, Shinyanga na Njombe kwa gharama ya Shilingi Bilioni 3 kila mkoa.
May be an image of 5 people, people standing, people sitting and indoor
May be an image of 12 people, people standing, people sitting and indoor
May be an image of 7 people, people sitting, people standing and indoor
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: OFISI YA RAIS TAMISEMI
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Ijumaa Machi 24,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
October 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Sep   Nov »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In