Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba pamoja na viongozi wa wilaya ya Manyoni ametembelea mashamba ya pamoja ya Korosho wilayani humo na kuridhishwa na undelezwaji wa kilimo hicho mkoani Singida.
Imekuwa ikizoeleka kilimo hicho kikifanyika zaidi katika nyanda za Kusini haswa mkoani Mtwara ambako ndipo wakazi wake wengi hutegemea zao ilo kujipatia kipato cha kujikimu katika maisha yao ya kila siku, kwa sasa hata Mkoani Singida kumekucha na Uwekezaji wa Kilimo hicho kutokana na Mnyororo wa thamani yake umekuwa na mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa.