“Pamoja na ukubwa tulionao Afrika lakini ni lazima tutawale soka la ndani
Lazima vilabu vya ndani vituogope kama wanavyotuogopa wengine huko nje
Hapo ndo inakuja umuhimu wa kushinda mchezo wa Jumapili ili kulinda heshima yetu”
–
“Haina maana kama unawafunga watu huko Afrika lakini humu ndani kuna timu inakusumbua. Ingawa tunajua wenzetu hii ndo World Cup yao, wachezaji wao waliwasajili kwa ajili ya mechi hii, viongozi wao mafanikio yao yanapimwa na mechi hii lakini jukumu letu kama Simba ni kutoruhusu watimize malengo yao kupitia sisi”
–
“Hatutataacha kitu Jumapili, hatupo tayari kuwapa faraja watu waliovunjika mioyo. Tunataka kuendeleza tabasamu kwa mashabiki wetu na tunataka kukaa kileleni tukiwa comfortable” Amesema Ahmed Ally, Msemaji wa Klabu ya Simba SC.