Lebo ya Konde Music Worldwide yake Harmonize imepewa siku mbili na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kuweka sawa yote waliyokubaliana na wasanii wake, Cheed na Killy katika mkataba endapo upande mmoja utasitisha mkataba kama walivyoandikishiana.
–
ADVERTISEMENT
Ofisa Sanaa Mwandamizi wa Basata, Abel Ndaga amebainisha hayo katika kikao cha pili kilichopangwa kukutanisha pande zote mbili baada ya kikao cha kwanza kilichopangwa Oktoba 12, 2022 ambapo vikao vyote msanii Harmonize hakuweza kuhudhuria.
ADVERTISEMENT