Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Dar es Salaam yatakosa umeme kwa saa 8 leo Jumatatu Oktoba 24, 2022 kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 8 mchana.
Taarifa iliyotolewa leo na Shirika hilo imetaja sababu ya kukosekana nishati hiyo ni kutokana na matengenezo yanayotarajiwa kufanyika ya mtambo namba mbili wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Songas uliopata hitilalfu.
–
“Shirika limepanga kufanya matengenezo ya mtambo namba mbili (2) wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Songas uliopata hitilafu. Matengenezo haya yamepangwa kufanyika siku ya Jumatatu Oktoba 24, 2022 kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 8 mchana,” imesema taarifa hiyo na kuongeza.
–
“Iwapo matengenezo kwenye mtambo huu yatachelewa kufanyika, itasababisha madhara makubwa kwenye mtambo husika, hali itakayosababisha athari za upatikanaji umeme kwa muda mrefu.” Imesema taarifa hiyo.
–
Bila kutaja maeneo yatakayoathiriwa na matengenezo hayo, Tanesco imesema “Wakati wa matengenezo haya, baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam yataathirika kwa kukosa umeme.”