“Najua uwezo wako na sina shaka unaenda kuongeza kitu katika Tasnia ya habari katika eneo la football nchini.
–
@azamfcofficial wamepatia sana na hapa wamelamba dume kweli kweli, tunahitaji Watu wenye passion na Soka , tunahitaji watu watakaotuongezea thamani ya huu mchezo murua, tunawahitaji wasio na haraka ya umaarufu wao binafsi, Watu wapiganaji na wenye maono yenye maslahi na kandanda.
–
Niwaambie tena Azam. Hii ni best choice na itawalipa, Dogo hajawahi kukosa kuuliza kwa Wakubwa, ni mpeke peke mwenye faida na huo ni mtaji mkubwa kwa Club yake.
–
Kila la kheri Mpare mwenye adabu zake, usije kuniangusha mwanangu, Ukienda ndivyo sivyo ntakuja na viboko nikuchape mbele ya @husnabona ” Ameandika @hajismanara kwenye IG Yake