Baadhi ya mashabiki wa timu ya Club Africain ya Tunisia wameonesha hofa yao kwa Mshambuliaji Fiston Mayele baada ya timu hiyo kupangwa kucheza na Yanga katika mchezo wa mtoano wa kutafuta timu zitakazoingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika.
–
Kupitia maoni (comment) katika ukurasa wa timu hiyo baadhi ya mashabiki wameonesha hofu yao kwa mshambuliaji Fiston Mayele kuwa ni mchezaji hatari na wa kuchugwa sana katika mchezo wao wa kwanza utakaopigwa Novemba 02, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
–
“Nguvu ya timu ya Tanzania (Yanga SC) ipo kwa mshambuliaji wa Congo, Kalala Mayele tu. Mshambuliaji huyu anatakiwa kuchugwa sana na akidhibitiwa hakuna hofu kwa klabu yetu ( Club Africain)” ameandika moja ya shabaki wa timu hiyo.
–
Mashabiki hao wameendelea kuichambua Yanga na kusema kuwa ni timu yenye wachezaji bora wenye nguvu na kasi hivyo sio ya kuidharau kuwa wataifunga kwa urahisi kama ilivyokuwa kwa timu ya Kipanga ya Zanzibar walioifunga bao 7-0.
–
Fiston Mayele alimaliza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na mabao 7 katika michezo 4. Mabao 6 kati ya hayo alifunga dhidi ya Zalan FC.