Mchezaji wa mpira wa Rugby katika Ligi ya Australia Liam Hampson (24), amekutwa akiwa amekufa nchini Hispania baada ya kupotea wakati akiwa ametoka usiku na marafiki zake.
–
Liam alikuwa na kundi wakiwemo wachezaji wa Ligi ya Taifa ya Mpira wa Rugby kwenye matembezi ya mwisho wa msimu.
–
Jumanne alfajiri, wakati wachezaji hao wakitoka katika klabu ya Sala Apollo mwanamichezo huyo hakuonekana ,hivyo baadaye wenzake waliripoti kupotea kwake.
–
Mwili wa Liam ulikutwa Jumatano mchana na wafanyakazi wa klabu hiyo ukiwa kwenye sakafu katika jiji la Barcelona.
–
Inasadikiwa kuwa kijana huyo alianguka kwa bahati mbaya kutoka kwenye urefu wa takribani mita 10.
–
Alikuwa akiichezea klabu ya Redcliffe Dolphins katika kombe la Queensland.