ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Mlinzi wa klabu ya Arsenal Pablo Mari (29) amelazwa hospitali baada ya shambulio la kitu chenye ncha kali ambalo limesababisha kifo cha mtu mmoja.
–
Mari ambaye anaichezea klabu ya Monza ya nchini Italia kwa mkopo alikuwa kati ya watu sita walioshambuliwa wakiwa kwenye eneo lenye maduka mengi katika Jiji la Milan.
–
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Klabu ya Monza Adriano Galliani, Mari alichomwa na kitu mgongoni. Jeraha lake limeacha shimo refu lakini kwa bahati kitu kilichotumika kumchoma hakikugusa viungo vingine.

Hivi sasa anapatiwa matibabu ya dharura na najitambua, kwa mujibu wa madaktari jeraha lake halihatarishi maisha yake na wanatarajia baada ya matibabu stahiki,atapona.