
Golikipa wa Singida Big Stars, Metacha Mnata amemuomba radhi mchezaji Charles Ilanfya wa Mtibwa Sugar kutokana na kumfanyia kitendo ambacho sio cha kiungwana.
–
“Nimejaribu kukupigia simu tangu jana baada ya mchezo lakini kwa bahati mbaya sikupati hewani. Nimeona nikuombe radhi hadharani kwa tukio lisilo la kiungwana nililokutendea katika mchezo wetu uliopita.
–
”Natambua kosa na kulijutia hivyo naamini utanisamehe wewe binafsi, mashabiki wa Mtibwa Sugar nao watanisamehe, mashabiki wangu na mashabiki wa Singida Big Stars, viongozi wetu pamoja na wadau wote kwa sababu mpira wa miguu ni mchezo wa burudani na sio uadui,” ameandika Metacha kwenye ukurasa wake wa IG
–
Ilanfya amejibu kwa kumwambia; “Yamekwisha ndugu yangu, sisi sote ni familia moja,”