Mwasisi aliyelipigania Taifa la Tanzania (Tanganyika) kuwa taifa huru na ikawezekana mwaka wa 1961 ambaye pia ni Rais wa kwanza wa zamani wa Taifa hilo Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ametajwa kuwa katika rekodi ya miongoni mwa viongozi Barani Afrika waliosoma katika chuo kikuu cha Makerere kilichopo katika mji mkuu wa Kampala nchini Uganda ambacho kwa sasa kimetimiza miaka 100 tangu uanzilishi wake. Kupitia Ukonwe wa chuo hicho na kufanikisha Viongozi wakubwa kwa maarifa waliyoyapata kupitia mafunzo yake, kimejiletea umaarufu mkubwa uliaja ufanisi wake katika masuala ya Utoaji wa Elimu bora.
Aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu pia wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati William Benjamini Mkapa nae ni moja ya viongozi waliosoma chuo hicho akitokea nchini Tanzania