Muuguzi (Nesi) ameshitakiwa kwa kuuwa watoto 7 na wengine 10 kuponea chupuchupu. Mojawapo ya viapo vya wataalam wa afya ni kwamba siku zote hawatafanya jambo lolote la kudhuru mgonjwa, lakini hali imekuwa kinyume huko Uingereza.
–
Lucy Letby aliyekuwa muuguzi kwenye wodi ya watoto wachanga anashitakiwa kwa makosa ya kuuwa watoto 7 kwa makusudi na kujaribu kuuwa vichanga wengine 10.
Inadaiwa nesi huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa akiwachoma watoto wachanga sindano iliyojazwa hewa na wengine aliwachoma sindano ya kushusha sukari (insulin).
–
Watoto wengi wanaodiwa kuuwawa na nesi huyo walikuwa njiti. Mara kadhaa nesi huyo alikuwa akiomba kwa wasimamizi wake kwamba anaomba amhudumie mtoto fulani, masaa kadhaa baadae mtoto huyo alikuwa anakufa.
–
Kesi ya nesi huyo ambayo inasikilizwa katika mahakama ya Manchester huko Uingereza imekuwa kama filamu ya kutisha jinsi mwanamke huyo alivyokuwa anatekeleza mauaji ya vichanga hao ambao hawana hatia yoyote.