Mwanamke mmoja katika jimbo la Jambi nchini Indonesia ameuawa na kumezwa na chatu, Jahrah, anayeripotiwa kuwa na umri wa miaka 50, alikuwa ameelekea kazini katika shamba la mpira Jumapili asubuhi.
–
Aliripotiwa kutoweka baada ya kushindwa kurejea usiku huo, ambapo msako wakujua alipo ulianza mara moja. Siku moja baadaye wanakijiji waligundua chatu mwenye kile kilichoonekana kuwa tumbo kubwa. Baadaye wenyeji walimuua nyoka huyo na kuukuta mwili wake ukiwa ndani.
–
Mkuu wa polisi wa Betara Jambi AKP S Harefa aliviambia vyombo vya habari vya nchi hiyo kwamba “Mwathiriwa alipatikana tumboni mwa nyoka huyo,” , akiongeza kuwa mwili wake ulionekana kuwa sawa kwa kiasi kikubwa ulipopatikana.
–
Alisema mume wa marehemu jumapili usiku alikuta baadhi ya nguo zake na zana alizotumia katika shamba la mpira .
–
Baada ya nyoka huyo mwenye urefu usiopungua mita 5 (futi 16) kuonekana Jumatatu, wanakijiji kisha wakamkamata na kumuua ili kuthibitisha mwili wa mwanamke huyo.