Ndege ya Shirika la Ndege la Korean Air jana usiku ilipata ajali baada ya kupitiliza njia wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mactan-Cebu nchini Philipines.
–
Ndege hiyo aina ya Airbus SE A330 iliyokuwa ikisafiri kutokea Seoul kwenda Cebu ilijaribu mara mbili kutua wakati hali ya hewa ikiwa mbaya na ilikwama.
ADVERTISEMENT
–
ADVERTISEMENT
Wakati ikijaribu kutua kwa mara ya tatu ndipo ilipopata ajali. Watu wote 173 wakiwemo abiria na wahudumu waliokolewa wakiwa salama.