Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), limethibitisha kuwa mwanafunzi wa darasa la 7 Iptisum Suleman Slim, alibadilishiwa namba ya mtihani na uchunguzi umepelekea kugundulika kwa wanafunzi wengine 7 kubadilishiwa namba zao za mitihani, na kuchukua hatua ya kuifungia shule ya Chalize Modern kuwa kituo cha mitihani ya baraza hilo.
ADVERTISEMENT
–
Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof.Adolf Mkenda, amesema uchunguzi umebaini taarifa zilizotolewa na mwanafunzi huyo ni kweli.
ADVERTISEMENT