Klabu ya Wolves imesema kwamba mshambuliaji wao raia wa Ureno, Pedro Neto, hatoshiriki Kombe la Dunia la 2022 kwa sababu anahitaji kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.
–
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, aliumia katika mchezo wao dhidi ya West Ham Jumamosi iliyopita Oktoba 1, alipotolewa baada ya dakika 24 kutokana na jeraha hilo.
–
“Kutokana na tathmini zaidi na maoni ya mtaalamu, wiki hii imepangwa kufanyiwa upasuaji. Hii ina maana kwamba, kwa bahati mbaya, hatokuwa sawa kwa Kombe la Dunia lijalo.”” taarifa ya klabu iliongeza.
Neto ameichezea Ureno mara tatu alipokuwa kwenye kikosi chao kwa mechi za hivi karibuni za Ligi ya Mataifa dhidi ya Jamhuri ya Czech na Uhispania hakucheza pia.
–
Kombe la Dunia litafanyika kuanzia Novemba 20 hadi Disemba 18 nchini Qatar.