Mwanadada Gifty Ohemaa kutokea nchini Ghana ambaye anafanya biashara ya ngono (changudoa) amesema hadi sasa amelala na Wanaume zaidi ya 1000 katika kazi yake hiyo.
–
Akihojiwa na SVTV Africa, Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 22 amesama changamoto kubwa ya kazi hiyo Ni kufanya vitendo vya udhalilishaji na hata kuibiwa kwani wanafanya kazi nyakati za usiku.
–
“Kuna siku nikiwahi kubakwa na Wanaume 8 kwa mpigo na kisha kuniibia vitu vyangu” alisema Ohemaa
–
Ameendelea kusema kuwa sio kwa mara ya kwanza kufanyiwa hivyo kwani aliwahi pia kubakwa na moja ya Dereva tax.
–
Mwanadada huyo amesema Ni ngumu kwake kuacha kazi hiyo japo anaelewa kujiuza ni kazi hatari kwa afya na hata kwa maisha yake kwa ujumla.