Baada ya Msanii Harmonize (Rajab Kahali) kuandika kupitia kurasa za mitandao ya kijamii kwa kumuhusisha msanii kutokea nchini Nigeria Burna Boy kuwa ndie msanii anayefanya poa sana Barani Afrika, imeibua maswali mengi hapo kwa umma kutaka kufahamu zaidi maoni au mitazamo ya wadau kuhusu utofauti uliopo kati ya Msanii bora na Msanii mkubwa. Je kwa upande wako maoni yapi unaweza kutoa juu ya kutambua utofauti uliopo kati ya Msanii bora na msanii mkubwa< Ikiwa mtazamo wa haraka ni kwamba Msanii bora ni msanii anayezingatia utunzi sahihi wa mashahiri kwa kuzingatia matumizi mazuri ya lugha iliyo fasaha kwa dhumuni kuu la kuelimisha jamii inayomzunguka na mara nyingi tunzi zao huishi kwa miaka mingi bila ya kuchuja lakini kwa upande wa Msanii Mkubwa ni msanii ambaye anaweza pia akawa bora au sio bora katika utunzi na matumizi ya lugha fasaha kwa lengo ila anakuwa na umaarufu mkubwa kwa kujizolea mashabiki wengi ndani na nje ya mipaka ya nchi aliopo kwa sababu ya utunzi wa nyimbo zinazochangamana na watu wa jamii tofauti kwa kuzingatia soko la muziki linahitaji ladha au vionjo nya muziki wa namna gani, haya sasa ni zamu yako kutililika kuhusu hili.