ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

NMB yazindua kampeni maalumu kufanikisha msimu mpya wa korosho 

I am Krantz by I am Krantz
Oct 13, 2022
in HABARI
0
NMB yazindua kampeni maalumu kufanikisha msimu mpya wa korosho 
0
SHARES
44
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

–

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed (katikati) akimkabidhi kadi ya pikipiki kiongozi wa chama cha msingi kutoka mkoani Mtwara moja ya pikipiki kama ishara ya kuzindua rasmi kampeni ya Bonge la Mpango Mchongo wa kusini itakayo husisha vyama vya msingi vya wakulima wa korosho mkoani Mtwara na Lindiå. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini, Bi. Janeth Shango na wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa benki ya NMB, Bw. Isaac Masusu.

RelatedPosts

Waziri Dkt. Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Waziri Dkt. Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Jan 25, 2023

🔴 #LIVE : NMB AWARDS SHOWCASE – NOV 23, 2022

Nov 23, 2022

NMB yapongezwa kusaidia Wakandarasi- Zanzibar

Nov 16, 2022
Load More

Msimu wa mwaka huu wa korosho unaanza rasmi tarehe 14 Oktoba 2022 ukilenga uzalishaji wa tani 400,000 za zao hilo lengo ambalo Benki ya NMB imesema iko tayari na ina uwezo kifedha kuhakikisha linafanikiwa.

Katika kutimiza azma hiyo, jana benki hiyo ilibainisha utayari wake wa kufanya hivyo na kubainisha mikakati iliyonayo kulisaidia taifa kupata matokeo chanya kwenye msimu huu wa 2022/23.

Mbali ya mikopo na huduma zake nyingine, NMB inapanga kutumia kampeni maalumu ya kuhamasisha matumizi ya benki kuufanya msimu huu mpya kuwa wa mafanikio makubwa zaidi kiuzalishaji na kibiashara ikilinganishwa na msimu iliyopita.

Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa benki hiyo, Bw. Isaac Masusu, amezindua kampeni ya “Bonge la Mpango – Mchongo wa Kusini” na mchakato mzima unawalenga wakulima wa korosho na vyama vya ushirika (AMCOS) kwenye Kongamano na Viongozi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Mtwara ililoliandaa kwa ajili ya kubadilishana mawazo jinsi ya kuufanikisha msimu huu na wadau wa zao hilo.

ADVERTISEMENT

 

Bw Masusu alisema pia kongamano hilo limefanyika kwa kutambua ambavyo kilimo cha korosho kimekuwa nguzo muhimu kwa ustawi wa Kanda ya Kusini hususani mikoa ya Lindi na Mtwara lakini pia kwa taifa na hata Benki ya NMB.

Aidha, alisema kuwa wakulima watakaotumia NMB kufanya malipo ya mauzo yao wataziwezesha AMCOS zao kushinda zawadi zilizotengwa kwa ajili ya kampeni hiyo ambayo zawadi zake ni pikipikitano watakazozipata washindi kwenye droo zitakazofanyika kila baada ya wiki mbili.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, alisema kampeni hiyo itasaidia sana kubadilisha maisha ya watu wengi na kutoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa korosho wa Mkoa wa Mtwara  inaendana na juhudi za serikali za kurasimisha miamala na kuongeza matumizi ya mifumo ya kibenki, vitu ambavyo ni muhimu kwenye utekelezaji wa agenda ya taifa ya kuendeleza huduma jumuishi za kifedha nchini.

Droo yake ya kwanza itafanyika October 28 mwaka huu. Mbali na kuwahamasisha wakulima kuitumia zaidi benki ya NMB kufanya miamala, sababu nyingine za kampeni hiyo ni kuhamasisha amana na kuwasaidia watu kuweka akiba.

 

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

ADVERTISEMENT

MWISHO…

 

Related

Tags: NMB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Ijumaa Machi 24,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
October 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Sep   Nov »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In