Mwanamuziki Nuh Mziwanda, leo, amefunguka na kusema anawashangaa wasanii wanaotoka kwenye lebo (usimamizi), wakati huko kuna afadhali kuliko kujisimamia mwenyewe.
–
@iam_mziwanda ameenda mbali zaidi na kusema kuwa ameshindwa hata kuachia EP (Extended Playlist) yake kutokana na kukosa usimamizi.
–
“Mimi nilitangaza kuachia EP ila mpaka sasa ishakua BP kwangu 😂 maana kila mtu ana mtu wake, Nawaonea huruma sana mnaotoka kwenye Usimamizi 😔 Ameandika @iam_mziwanda
–
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii mbalimbali kuvunja mkataba na lebo zilizokuwa zinawasimamia kwa sababu mbalimbali ambazo nyingi hazijawekwa wazi.