Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Mkoa wa Temeke, (TEFA) Peter Mhinzi amefariki dunia alfjiri ya leo Oktoba 03, 2022.
–
Peter Mhinzi amefariki Dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
–
Afisa Habari wa Chama hiko, Ben Mwanantala amethibitisha kutokea kwa kifo hiko na amewaomba wadau wa soka mkoa wa Temeke na Watanzania wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu.
–
Kwa sasa Msiba upo nyumbani kwa Marehemu Tandika Temeke Mtaa wa Ngomano, Dar es Salaam.