Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amewaomba msamaha Wakenya na Afrika Mashariki kwa Ujumla kufuatia mtafaruku uliosababishwa na mtoto wake, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika ujumbe wa kwamba yeye na jeshi lake wanaweza kuliteka Jiji la Nairobi kwa wiki mbili
–
Pia Rais Museveni ameeleza sababu za kumpandisha cheo Muhoozi kutoka kuwa Luteni Jenerali na kumpa Ujenerali licha ya kauli hizo
–
“ametenda vibaya kama afisa wa Umma. Hata hivyo kuna michango mingine mingi chanya ambayo Jenerali ametoa na bado anaweza kutoa. Naomba ndugu zetu wa Kenya watusamehe kwa tweets alizotuma Jenerali Muhoozi.” – Rais Museveni