ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Profesa Said Shehe Aboud kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
–
Profesa Aboud ni Profesa Mshiriki na Kaimu ¹Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dar es Salaam.
–
Profesa Aboud anachukua nafasi ya Profesa Yunus Mgaya ambaye amemaliza muda wake mwezi Septemba mwaka huu.
–
Uteuzi wa Profesa Aboud umeanza tarehe 19 mwezi huu.